Pata taarifa kuu
LA FRANCOPHONE

La Francophonie: Hatuingilii uhuru wa nchi lakini tunalinda demokrasia na haki

Mabalozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa nchini Tanzania, hii leo wamezindua rasmi wiki ya La Francophone huku wakisisitiza kuhusu kuheshimiwa kwa haki za binadamu, demokrasia, amani pamoja na tamaduni.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederick Clavier akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Francophone. 18 Machi 2019, picha kwa hisani ya Le Mutuz Blog
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederick Clavier akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Francophone. 18 Machi 2019, picha kwa hisani ya Le Mutuz Blog RFI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na idhaa hii kando na uzinduzi wa wiki ya La Francophone, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederick Clavier, amesema Jumuiya ya La Francophone inaongozwa na misingi mikuu minne ambayo ni utamaduni, amani, demokrasia na haki za binadamu, mambo ambayo amesema nchi wanachama zimeendelea kusimamia.

Balozi Clavier amesema licha ya kuwa jumuiya hiyo inahamasisha ulinzi wa haki za binadamu na demokrasia, haiingilii uhuru wa nchi kufanya maamuzi katika masuala haya mbali ya kukemea kwa kuwa hata Ufaransa yenyewe inakabiliwa na changamoto hizo.

Ndio, kwa pamoja tunajaribu kulinda baadhi ya desturi kama vile demokrasia, haki za binadamu..na tunajua kuwa sio rahisi hata nchini mwangu! Ukweli ni kuwa La francophone inajaribu kufanya kazi ya kujenga uwezo kwa nchi wanachama kutetea demokrasia, kwa sababu hatupo kutengeneza mchezo wa kivita dhidi ya nchi nyingine, tunachofanya ni kushirikiana kazi kwa pamoja”.

Balozi Clavier amesema mbali na utamaduni, jumuiya hiyo imekuwa ikihamasisha hata nchi ambazo hazitumii lugha ya kifaransa kujiunga kama waangalizi kwa kile alichosema ndani ya jumuiya kuna fursa za kiuchumi na uwekezaji ambazo wanaweza kutumia.

Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abid Benryane akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu wiki ya Francophone. 18 Machi 2019
Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Abid Benryane akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu wiki ya Francophone. 18 Machi 2019 RFI

Kwa upande wake balozi wa Morocco nchini Tanzania Abid Benryane ambaye ndie mwenyekiti wa jukwaa hilo kwa mwaka huu, amesema lugha ni kiungo muhimu kinachiunganisha mataifa akitoa wito kwa watu kujifunza lugha zaidi ya moja.

Napenda ni nikuu maneno ya mfalme Hassan wa pili wa Morocco, alikuwa akisema..kwangu mimi ujinga ni mtu kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha moja peke yake. Nguvu ya Francophone ni kuwa, kupitia lugha tumepata mafanikio makubwa katika nyanja ya ushirikiano wa kimataifa”.

Maadhimisho ya mwaka huu nchini Tanzania yataambatana na maonesho ya filamu, muziki, utamaduni wa chakula na michezo kama sehyemu ya kuhamasisha utangamano na umoja baina ya nchi wanachama na zile ambazo si wanachama wa jumuiya hiyo.

La Francophone inaundwa na mataifa 88 duniani huku ikikadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni 300 duniani wanazungumza kifaransa kama lugha ya mawasiliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.