Pata taarifa kuu
RWANDA-USAFIRI-USALAMA

Rwanda yapiga marufuku Boeing 737 Max kuruka katika anga yake

Rwanda imejiunga na mataifa mengine duniani kupiga marufuku usafiri wa ndege aina ya Boeing 737 Max 8 na Max 9.Hatua hii inakuja baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157.

Boeing 737 ya shrika la ndege la Ethiopia Alirlines kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Addis Ababa.
Boeing 737 ya shrika la ndege la Ethiopia Alirlines kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Addis Ababa. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ni ajali ya pili ya aina hiyo ya ndege ya 737 Max katika muda wa miezi mitano.

Baadhi ya watu wamegusia ufanano wa mikasa hiyo, huku baadhi ya wataalamu wakitaja data ya satelaiti na ushahidi kutoka eneo la mkasa kuonyesha uhusiano wa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile ya iliyotokea Indonesia ya Lion Air mwaka jana.

Ndege ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.

Mamlaka ya usafiri wa ndege nchini Rwanda (RCAA) imetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ana 9 katika anga ya Rwanda.

Kwa mujibu wa chanzo kutoka mamlaka ya usafiri wa ndege la Rwanda, RCAA, Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina ya Boeing 737- 800.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.