Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-MAUAJI-USHIRIKIANO

Mauaji ya kimbari Rwanda: Afisa wa zamani wa jeshi la Ufaransa atoa ushahidi mpya

Afisa wa zamani katika ngazi ya juu ya jeshi la Ufaransa, Jenerali Jean Varret, ametoa ushahidi mpya kuhusu msimamo wa Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda.

Gari la askari wa Ufaransalikipita karibu na wanamgambo wa Kihutu wa Interahamwe Juni 27, 1994 karibu na Gisenyi, magharibi mwa Rwanda
Gari la askari wa Ufaransalikipita karibu na wanamgambo wa Kihutu wa Interahamwe Juni 27, 1994 karibu na Gisenyi, magharibi mwa Rwanda © AFP PHOTO / PASCAL GUYOT
Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyo wa zamani wa ujumbe wa ushirikiano wa kijeshi wa Ufaransa nchini Rwanda amesema alipinga msaada wa Ufaransa kwa rais Habyarimana, bila mafanikio.

Kwa mujibu wa afisa huyo mwenye umri wa miaka 84, mkuu wa polisi ya Rwanda wakati huo, Kanali Pierre-Célestin Rwagafilita, alimwambia mnamo mwaka 1990 kwamba Watutsi walio wachache wanatakiwa "kuangamizwa". Jenerali Jean Varret ametoa ushahidi huo kwa wenzetu wa redio France Inter na Médiapart. Ni karibu miaka 25 sasa baada ya mauaji hayo yaliyotokea nchini Rwanda, ambapo Jean Varret anaamua kuvunja ukimya na kusema yalityotokea huku akieleza jukumu la Ufaransa wakati wa maujai hayo.

Amerejelea hasa mazungumzo ya ana kwa ana kati yake na afisa wa polisi ya zamani ya Rwanda , Pierre-Célestin Rwagafilita: "Na hapo, aliniambia: 'Tunaongea ana kwa ana, sote hapa ni askari, tunapaswa kuweka mambo yote wazi. Ninakuomba hizo silaha, kwa sababu nitashiriki na jeshi katika operesheni ya kuondoa njiani tatizo hilo'. Niliposhangazwa na kauli hiyo, alisema: 'Tatizo hilo, ni rahisi sana. Ukweli ni kwamba Watutsi sio wengi, tutawaangamiza'. Alinambia wazi. "

Kwa upande wa Jenerali Varret, amesema mpango wa mauaji ya kimbari ulikuepo. Anasema pia kuwa alitoa taarifa hiyo kwa jeshi la Ufaransa, lakini viongozi hawakujibu: "Hakuna. Kwa sababu hawakutaka kuunga mkono mpango huo wa Habyarimana. Kwa bahati mbaya, historia imethibitisha kwamba ilikuwa ni kosa, zaidi ya kosa, kwa sababu mauaji ya kimbari yalitokea bila hata hivyo kuzuia kabla hayajatokea wakati taarifa za mpango huo zilikuepo.

"Mwezi ujao, Rwanda inajiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari. Rais wa Ufaransa amealikwa rasmi kwenye sherehe hizo. Elysee mpaka sasa, haijaweka wazi jibu lake. Emmanuel Macron alijibu tu kwamba Ufaransa itawakilishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.