Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA

Kauli ya Kagame kuhusu mauaji ya mwanasisa wa upinzani yazua sintofahamu

Kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Sth Sendashonga imezua hali ya sintofahamu nchini humo. Hivi karibuni rais wa Rwanda alizungumzia kuhusu mauaji ya mwanasiasa huyo ambaye alimshtumu kwamba alikuwa na lengo la kuipindua serikali yake.

Paul Kagame, rais wa Rwanda, hapa ilikuwa katika Mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia, Novemba 2018 (picha ya kumbukumbu).
Paul Kagame, rais wa Rwanda, hapa ilikuwa katika Mkutano wa Umoja wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia, Novemba 2018 (picha ya kumbukumbu). © AFP
Matangazo ya kibiashara

Seth Sendashonga ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani aliuawa kwa sababu alivuka mstari mwenkundu baada ya kutafuta uungwaji mkono kutoka majenerali wa Uganda.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na Uganda umeiendelea kuwa na dosari, ambapo Rwanda inamshtumu jirani yake kuwa inalenga kuwasaidia waasi wa kundi la RNC wanaoongozwa na Kayumba Nyamwasa kuhatarisha usalama wa Rwanda.

Baada ya kauli hiyo, familia ya Seth Sendashonga imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa kuchukuwa hatua wakati wanasiasa wa upinzani wanaendelea kuuawa nchini Rwanda.

Siku ya Jumapili, Paul Kagame alitetea moja ya vitabu vya mtafiti kutoka Ufaransa, Gerard Prunier, ambaye aliandika, kwa mujibu wa rais wa Rwanda, kama sababu ya mauaji ya Seth Sendashonga mnamo mwaka 1998 mikutano na majenerali wa Uganda kwa lengo la kupindua serikali ya Kigali. "Kuna ushahidi tosha kwa yale alioandika Prunier, tulikuwa na taarifa hiyo. Kwa kweli, Seth Sendashonga aliuawa kwa sababu alivuka mstari mwekundu. Sina mengi zaidi ya kusema, lakini sitaomba msamaha kwa hilo, "alisema rais wa Rwanda.

Mnamo Mei 3, 1998, Seth Sendashonga alikutana na Salim Saleh, ndugu wa rais wa Uganda Yoweri Museveni. Tarehe 16 Mei, aliuawa na kundi la watu jijini Nairobi, nchini Kenya.

Machi 10, wakati Paul Kagame alitoa kauli hiyo mwanasiasa mwengine wa upinzani Anselme Mutuyimana, msaidizi wa kiongozi wa chama cha upinzani cha UDF, cha Victoire Ingabire, aliokotwa maiti nchini Rwanda. Polisi ya Rwanda inasema imeanzisha uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.