Pata taarifa kuu
KENYA-ETHIOPIA-BOEING

Raia 32 wa Kenya waangamia katika mkasa wa ajali ya ndege ya Ethiopia, iliyoua watu 157

Raia 32 wa Kenya ni miongoni wa abiria wote 157 waliopoteza maisha kufuatia ajali ya ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi nchini Kenya. 

Mabaki ya ndege ya Ethiopia Boeing 737 iliyopata ajali nchini Ethiopia na kuua watu 157
Mabaki ya ndege ya Ethiopia Boeing 737 iliyopata ajali nchini Ethiopia na kuua watu 157 Ethiopia Airlines
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea mapema leo asubuhi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Uwanja wa ndege wa Bore Mjini Adis Ababa.

Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema ndege hiyo ilibeba abiria kutoka mataifa 32 yakiwemo Marekani, Uingereza, China, India, Misri, Canada na Ufaransa

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

Katika hatua nyingine, Waziri wa usafirishaji wa Kenya, James machari amesema serikali ya nchi hiyo imepeleka maofisa kadhaa eneo la ajali na kuwataka raia kuwa watulivu.

Katika hatua nyingine shirika la Marekani la Boeing lililotengeneza ndege hiyo limeeleza kusikitishwa kwake na ajali hiyo iliyoua abiria wote na kuongeza kuwa litatoa msaada wa kiufundi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Ndege hiyo mpya aina ya Boeing 737 ambayo ilinunuliwa mwaka jana ilikua ikitokea jijini Addis Ababa kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kabla ya kuanguka muda mfupi baada ya kuruka.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.