Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-UGANDA

AFD na AKDN wafanikisha kuanza kufanya Upasuaji wa Kisasa wa Moyo Tanzania

Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD limesema litaendelea kushirikiana na Serikali za nchi za Afrika Mashariki katika sekta ya Afya hasa katika Misaada Miundo mbinu na wataalam.

Jengo Jipya la Agakhan Dar es salaam
Jengo Jipya la Agakhan Dar es salaam Picha Agakhan
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mara baada ya kuzindua jengo Jipya la Hospitali ya Agakhan Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa shirikila hilo katika kanda ya Afrika Mashariki Christian Yoka ansema bila ubora wa huduma ni vigumu kutoa huduma stahiki za afya.

''Unahitaji kufanyia kazi ubora wa huduma zinazotolewa moja kati ya mambo ambayo tunajaribu kuyafanikisha ni namna ya kuhakikisha wananchi wanaweza kumudu kupata huduma za afya” alisema Christian Yoka

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Afya wa Shirika la Maendeleo la Agakhan Duniani AKDN Dakta Gijs Walraven anasema AFD wamesaidia ili kutoa matibabu kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Akizungumzia Umuhimu wa Hospitali hiyo, Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa mara baada ya kulizindua anasema ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi utawasaidia ananchi kupata huduma bora.

Jengo hilo hilo jipya limesheheni vifaa vya kisasa,vitakavyosaidia kupata matibabu ya Magonjwa ya Saratani,Moyo, Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu na Ubongo pamoja na Huduma za afya ya uzazi kwa mama na Mtoto.

Dakta Mugisha Mazoko ni mmoja wa Madktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo anasema bado kuna uelewa finyu miongoni mwa wananchi kuhusu upasuaji.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederick Clavier anasema serikali ya Ufaransa imewekeza kiasi cha Dola Milioni 53.5 kimkakati huku Jengo hilo likigharimu Dola Milioni 83.5.

02:03

STEVEN MUMBI Akiripoti Kuhusu Kufunguliwa Jengo Jipya la HOSPITALI AGHAKAN TANZANIA 09 MARCH 2019

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.