Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Wanafunzi UDSM Kunufaika na Udhamini kwa kwenda kusoma Ufaransa

media Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier akifungua kituo cha taarifa UDSM Picha/Imani Nathanael

Serikali ya Ufaransa imeanza kutengeneza mazingira rahisi kwa wanafunzi kutoka nchi za Kiafrika kwenda kusoma barani Ulaya, miongoni mwa nchi zitakazonufaika ni Tanzania ambapo wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wataanza kunufaika na mpango huu kwenda kusoma shahada ya uzamili na uzamivu.

Hatua hiyo itawasaidia wanafunzi wa Chuo hicho kupata taarifa ya namna ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu vya Ufaransa kwa njia rahisi.

Kaimu Mkuu wa chuo William Anangisye anasema hatua hiyo ni muhimu kwa wanafunzi kwani wanatakiwa kutembelea ili kupata taarifa Muhimu.

Mbali na Chuo hicho chuo kitakachonufaika na mpango huo ni pamoja na Chuo kikuu cha taifa Zanzibar SUZA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia nchini humo, Dkt. Leonard Akwilapo anasema wanafunzi watanufaika endapo watazingatia fursa hiyo kwani kuna uhitaji Mkubwa wa Wanafunzi kusoma kifaransa huku waadhiri wa somo hilo watapata fursa ya kujiendeleza katika ngazi za Uzamili na uzamivu.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier anasema serikali ya Ufaransa imeongeza bajeti yake ili wanafunzi wengi zaidi wasome nchini humo.

"leo hii tuna kozi zipatazo 1000 katika vyuo vikuu vya Ufaransa,serikali ya ufaransa imeamua kuongeza udhamini waDola milioni 12 kwa ajili ya wanafunzi wapatao 15" alisema Balozi Clavier

Hivi karibuni Serikali ya Ufaransa ilitangaza kuongeza ada kwa wanafunzi wanaotoka nje ya umoja wa Ulaya mara kumi na sita zaidi kutoka €170 hadi €2,770 kwa mwaka

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana