Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-USALAMA

Kayumba Nyamwasa aishtumu serikali ya Rwanda kuwafanyia vitisho wapinzani

Mwanajeshi wa zamani wa Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa aliyekimbia nchi hiyo ameishtumu serikali ya Kigali kwa kuwatisha wapinzani.

Jenerali muasi katika jeshi la Rwanda (RDF) Faustin Kayumba Nyamwasa.
Jenerali muasi katika jeshi la Rwanda (RDF) Faustin Kayumba Nyamwasa. AFP/MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Nyamwasa ametoa kauli hii baada ya kiongozi wa mashataka nchini humo kutoa hati ya kimatifa ya kukamatwa kwake na viongozi wa muungano wa vyama vitano vya upinzani maarufu kama P5.

P5 inaundwa pia na chama cha Nyamwasa kinachofahamika kama RNC ambacho Kigali inasema ni kundi la waasi.

P5 ni jukwaa la vyama vya kisiasa vya upinzani nchini Rwanda ambavyo vinatuhumiwa kuanzisha uasi mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya serikali ya Rwanda, jambo ambalo limekuwa likikanushwa na jukwaa la vyama hivyo. Mwezi Julai mwaka jana, vyama hivyo viliomba kuandaliwa kwa mazungumzo ya kisiasa na rais Paul Kagame, ombi ambalo mpaka sasa halikupata jibu.

Jenerali Nyamwasa alikuwa mtu wa karibu sana na rais Paul Kagame ambae kwa sasa anaeshi nchini Afrika Kusini chini ya ulinzi mkali wa idara ya usalama nchini humo baada ya jaribio la kutaka kuuwawa mwaka 2010.

Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha RNC pamoja na vyama vingine wanatuhumiwa na utawala wa Kigali kuanzisha uasi mashariki mwa Congo katika eneo la Fizi na Uvira. Serikali ya Kigali imetaka Pretoria kumkamata Nyamwasa na kuzuia mali zake. Waranti hizo zimetolewa katika kipindi hiki kisichokuwa cha kawaida kati ya Rwanda na Congo na kati ya Rwanda na Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.