Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Ufaransa yazindua vituo vya Taarifa kwa wanafunzi wa Uzamivu Tanzania

media Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier alipotembelea Studio … Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frédéric Clavier akizungumza katika studio za RFI Kiswahili, Dar es Salaam. 22/05/2018 RFI Kiswahili

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amezindua vituo vya taarifa kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini humo wanaohitaji kwenda kusoma nchini Ufaransa katika kozi za Shahada ya uzamivu na Shahada ya Uzamilivu.

Balozi Clavier amesema vituo hivyo vya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar SUZA na kile cha utamadini cha Alliance Francee vitasaidia wanafunzi kupata taarifa kwa urahisi, lengo ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma nchini Ufaransa.

"Lengo lililowekwa na Rais Emmanuel macron ni Kuongeza Mara Mbili zaidi Idadi ya wanafunzi kutoka nchi nyingine, zaidi ya Vyuo 200 vya Elimu ya juu vinafundisha kwa lugha ya kiingereza katika fani mbalimbali" alisema Clavier.

Akizungumzia namna wakatavyokuwa wanatoa taarifa kwa Wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma vyuo vya eliumu ya juu Ufaransa Mkuu wa kituo cha Taarifa cha Alliance Francee kilichozinduliwa Karima Allaoui anasema kuwawekea mazingira rafiki ya kupata taarifa za vyuo.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu Sayansi na Teknolojia nchini humo Dakta Keneth Hossea alisema wanatarajia wanafunzi wengi watajitokeza kuchangamkia fursa hiyo.

Serikali ya Ufaransa imeongeza Bajeti yake na kufikia Dola za kimarekani Milioni 12 milioni kwa ajili ya kudhamini wanafunzi 15,000 wa kigeni kutoka Barani Afrika wanaohitaji kwenda kusoma elimu ya juu nchini humo lengo likiwa ni kufikia watu laki tano ifikapo mwaka 2027.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana