sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Hoteli ya kifahari yashambuliwa jijini Nairobi nchini Kenya

media Shambulizi katika hoteli ya Dusit jijni Nairobi, Kenya,lililotokea Januari 15 2019 REUTERS/Thomas Mukoya

Mlipuko mkubwa uliofuatiwa na milio ya risasi ilisikika Jumanne mchana katika hoteli moja Magharibi wa jiji kuu la Kenya Nairobi, katika shambulizi ambalo kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia linasema limehusika.

Ripoti zinasema kuwa, watu kadhaa wamejeruhiwa lakini idadi haijatajwa katika tukio hilo lililotokea katika hoteli hiyo inayofahamika kama Dusit.

Aidha, haijafahamika iwapo kuna watu waliopoteza maisha katika tukio hili ambalo jeshi la polisi linasema ni la  kigaidi.

“Leo mchana, karibu saa tisa hivi, watu wenye silaha walivamia eneo lililo na hoteli na ofisi na kufwatua risasi.Tunashuku ni tukio la kigaidi,” alisema Joseph Boinett Inspekta Mkuu wa jeshi la Polisi nchini humo.

“Maafisa wetu bado wanaendelea na operesheni ili kuwaondoa watu hao wenye silaha, lakini tayari tumewaokoa watu wengi sana,” aliongeza.

Wachambuzi wa masuala ya usalama, wanasema maafisa wa usalama wamejitahidi kushughulikia tukio hili kinyume na mambo yalivyokuwa wakati wa mashambulizi yaliyopita.

Shambulizi hili, limewakumbusha wengi shambulizi la kigaidi lilitokea mwaka 2013 katika jengo la biashara la Westgate na kusababisha vifo vya watu 67.

Mwezi Aprili mwaka 2015 shambulizi lingine la kigaidi lilitokea katika Chuo Kikuu cha Garissa Mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 148, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Kenya ilianza kushuhudia milipuko ya kigaidi kutoka kwa kundi la Al Shabab mwaka 2011, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia, kupambana na kundi hilo la kigaidi ambalo linapambana na serikali ya Mogadishu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana