Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-SOMALIA-USALAMA

Burundi yapinga uamuzi wa AU kupunguza askari wake 1,000 walioko Somalia

Burundi imesema haitakubali ombi la Umoja wa Afrika, kuwa ipunguze wanajeshi wake elfu moja walioko nchini Somalia katika kusimamia amani nchini humo baada ya kujiunga na kikosi cha umoja huo (AMISOM).

Askari wa Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kutoka Burundi wakipiga kambi kaskazini mwa Mogadishu tarehe 18 Novemba 2011.
Askari wa Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kutoka Burundi wakipiga kambi kaskazini mwa Mogadishu tarehe 18 Novemba 2011. REUTERS/Stuart Price
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Umoja huo ambao una kikosi cha kulinda amani nchini Somalia, AMISOM, uliiomba Burundi kupunguza wanajeshi wake 1,000 kufikia tarehe 28 mwezi Februari.

Msemaji wa jeshi la Burundi Kanali Floribert Biyereke amesema jeshi litaishauri serikali, kukataa ombi hilo na badala yake kupendekeza wanajeshi wa nchi zingine pia wapunguzwe bila kuangazia tu wale kutoka Burundi.

AU inasema, hatua ni kuhakikisha kuwa nchi zinazochangia wanajeshi nchini Somalia, zinakuwa na wanajeshi sawa.

Uamuzi huu unakuja wakati huu Burundi ikiendelea kuwa na uhusiano mbaya na Umoja wa Afrika kwa sababu ya mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

AMISOM inaundwa na wanajeshi kutoka mataifa matano yaukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambayo ni Uganda, Burundi, Ethiopia, Kenya na Djibouti.

Lengo likiwa ni kusaidia kurejesha amani nchini Somalia na kukabiliana na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Hili ni suala ambalo linatarajiwa kuzua mvutano zaidi kati ya AU na serikali ya Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.