sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Mazungumzo ya amani kuanza Sudan, rais …
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akiwa na mwenyeji wake rais wa Tanzania John Magufuli. 13 Juni 2019
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/06 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Burundi kuhamishia jiji kuu kwenda Gitega

media Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana

Burundi imetangaza kuwa makao makuu mapya ya nchi hiyo ni Gitega.

Bujumbura litasalia kuwa jiji la kibiashara huku mji wa Gitega unaopatikana katikati ya nchi hiyo, likiwa ndio makao mapya ya serikali na kisiasa.

Msemaji wa rais Pierre Nkurunziza, Jean-Claude Karerwa Ndenzako, kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, serikali sasa imeanza kutekeleza ahadi hiyo iliyotolewa na rais Nkurunziza miaka iliyopita.

“Mikutano ya Baraza la Mawaziri itakuwa inafanyika Gitega, na kuanzia mwaka 2019 Wizara tano zitahamia huko, Wizara ya elimu, Kilimo na Mambo ya ndani,” alisema.

Hata hivyo, bunge ambalo limetawaliwa na chama tawala cha CNDD FDD, linatarajiwa kupitisha uamuzi huo.

Mwaka 2007, rais Nkurunziza aliahidi kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Gitega mji ambao una idadi ya watu 30,000 na kuondoka jiji la Bujumbura ambalo lina watu Milioni 1.2.

Uamuzi huu hata hivyo umeshtumiwa kwa sababu Gitega haina miundo mbinu mizuri hasa hoteli au hata barabara, na inakuja baada ya serikali ya China kujenga Ikulu ya rais jijini Bujubura kwa kima cha Dola Milioni 20.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana