Pata taarifa kuu
EAC-USHIRIKIANO

Mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki waahirishwa

Wakati kukiripotiwa joto la mvutano na mgogoro ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa mara nyingine mkutano wa wakuu wa nchi uliokuwa umapengwa kufanyika juma lijalo jijini Arusha, Tanzania umeahirishwa.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (mbele) na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunziza (nyuma) ambao wanaendelea kushtumiana kila mmoja kutaka kuhatarisha usalama wa jirani yake.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (mbele) na mwenzake wa Burundi Pierre Nkurunziza (nyuma) ambao wanaendelea kushtumiana kila mmoja kutaka kuhatarisha usalama wa jirani yake. AFP PHOTO/JOSE CENDON
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalumu aliyofanya na idhaa ya Kiswahili ya RFI , mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Afrika Mashariki na naibu waziri mkuu wa Uganda Alhaji Dk Ali Chilunda, amesema mkutano wa Desemba 27 hautakuwepo na kwamba wenye mamlaka ya kutangaza tarehe nyingine ni wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hivi karibuni rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alimuandikia barua rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimueleza kutofurahishwa na nchi ya Rwanda anayoituhumu kuwaficha wahalifu waliojaribu kuipindua Serikali yake.

Mkutano huu ambao umeahirishwa kwa zaidi ya mara mbili, ulikuwa ufanyike mwezi Novemba jijini Arusha, lakini ukaahirishwa baada ya nchi ya Burundi kutotuma muwakilishi yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.