UGANDA-AFYA-EBOLA
Ebola: Uganda yaendelea na zoezi la upimaji wa Afya kwenye mpake wake na DRC
Serikali ya Uganda, imeendelea kuimarisha upimaji wa afya katika mpaka wake na DRC, kwa hofu ya kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kipindi hiki cha shamrashamra za Krismasi mji wa Mpondwe kwenye mpaka wa nchi hizo mbili upo hatarini kwa sababu ya kutembeleana kwa watu wanaovuka mpaka.
Aidha, Uganda inahofia kuwa iwapo ghasia zitazuka baada ya Uchaguzi wa Jumapili, wakimbizi huenda wakaingia nchini humo na kuhatarisha pia usambazaji wa Ebola.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukumbwa na ugonjwa hatari wa Ebola hasa mashariki mwa nchi hiyo, katika mkoa wa Kivu kaskazini.