Pata taarifa kuu
RWANDA-UBELGIJI-HAKI

Wanyarwanda 5 wafikishwa mbele ya mahakama Ubelgiji kwa uhalifu wa mauaji ya kimbari

Raia watano wa Rwanda wanaoshtumiwa kuhusika katika mauaji ya halaiki yaliyotokea nchini humo mwaka 1994, wamefikishwa mbele ya mahakama jinai nchini Ubelgiji kwa "uhalifu wa mauaji ya kimbari", Ofisi ya mashitaka ya Ubelgiji imetangaza.

Mabaki ya mtu aliyeuawa wakati wa mauaji ya kimbari kwenye eneo la kumbukumbu la Kigali, Rwanda.
Mabaki ya mtu aliyeuawa wakati wa mauaji ya kimbari kwenye eneo la kumbukumbu la Kigali, Rwanda. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

"Ni kwa mara ya kwanza mahakama ya jinai ya Ubelgiji kushughulikia kesi zinazohusiana na makosa ya mauaji ya halaiki," Ofisi ya mashitaka imesema katika taarifa yake.

Kesi nne zinazohusiana na mauaji ya kimbari ya Rwanda tayari zimesikilizwa nchini Ubelgiji kati ya mwaka 2001 na 2009, lakini kesi hizo zilihusu "uhalifu wa kivita," uliotekelezwa wakati huo, Ofisi ya mashitaka imekumbuka.

Mwishoni mwa mwaka 2009, Ephrem Nkezabera, anayefahamika kwa jina la "mdhamini wa mauaji ya halaiki", alihukumiwa kifungo cha miaka 30 na Mahakama ya jinai ya Ubelgiji.

Mahakama hiyo tayari imetoa hukumu kubwa kwa watawa wawili, mwanachuoni mmoja na mfanyabiashara mmoja mnamo mwaka 2001, wafanyabiashara wawili kutoka kaskazini mwa Rwanda mnamo mwaka 2005 na afisa wa zamani wa jeshi mnamo mwezi Julai 2007.

Kesi hii mpya inahusu watu watano waliokamatwa mwaka 2011.

Mwezi Machi 2011, watu wawili wenye asili ya Rwanda walikamatwa nchini Ubelgiji kwa madai ya "mauaji ya kimbari", "uhalifu wa kivita" na "uhalifu dhidi ya ubinadamu" kwa kuhusika kwao katika mauaji ya halaiki.

Kwa mujibu wa gazeti la Rwanda la New Times, watu hao ni Ernest Gakwaya, anayefahamika kwa jina la "Camarade", na Emmanuel Nkunzuwimye anayefahamika kwa jina la "Bomboko".

Mwezi mmoja baadaye, mnamo mwezi Aprili 2011, jaji wa zamani wa Rwanda, Mathias Bushishi, ambaye alikuwa akitafutwa na polisi ya kimataifa (Interpol) kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994,alikamatwa na kufungwa na kufungwa mjini Brussels.

Watu 800,000, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wengi wao kutoka jamii ya Watutsi waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.