Pata taarifa kuu
UGANDA-UCHUMI

Uganda kumchunguza waziri wake wa mambo ya nje kuhusiana na madai ya rushwa

Mamlaka nchini Uganda zitachunguza tuhuma kuwa waziri wake wa mambo ya nje, Sam Kutesa alipokea rushwa ya dola za Marekani laki 5 kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ya China.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mjini Kampala wakati akizindua mkakati mpya wa kupambana na rushwa, rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema waziri Mutesa alimueleza fedha hizo alichangiwa katika taasisi ya misaada anayoiongoza.

Kwenye hotuba yake rais Museveni amesema Serikali yake itazuia na kushikilia mali za viongozi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hatua hii ya Uganda inakuja baada ya nchi jirani ya Kenya kuanza kuwakamata na kuwafikisha mahakamani maafisa wa serikali wanaojihusisha na rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.