Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka

"Bw Patrice-Edouard Ngaisson amekamatwa na mamlaka ya Jamhuri ya Ufaransa kwa mujibu wa waranti uliyotolewa na Mahakama mwezi Desemba 2018, ICC imesema katika taarifa yake. Taarifa hii imethibitishwa na Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu kwa RFI.

E.A.C

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali ya boti nchini Uagnda yafikia zaidi ya 30

media Zoezi la kutafuta miili katika Ziwa Victoria nchini Uganda AFP

Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa boti katika Ziwa Victoria nchini Uganda, Jumamosi iliyopita, imefikia zaidi ya 30, wakati huu zoezi la kutafuta miili zaidi ikiendelea.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo Zura Ganyana amesema kuwa hadi sasa watu walionusurika ni 27 huku zaidi ya 60 wakiwa bado hawajapatikana.

Boti hiyo inaelezwa kuzama umbali wa mita 150 kutoka ufukweni na Sababu za kuzama zinaelezwa kuwa huenda ni idadi kubwa ya watu na hali mbaya ya hewa katika Ziwa hilo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesikitishwa na ajali hiyo. Ripoti za awali zinasema kuwa, boti hiyo haikuwa imesajiliwa na haikuwa na kibali maalum cha kufanya safara za maji.

Mauaji haya, yanakuja, miezi karibu miwili, baada ya watu zaidi ya 200 kupoteza maisha katka Ziwa hili nchini Tanzania.

Safari za maji katika Ziwa Victoria, zinaendelea kuwa hatari kutokana na uwezo mdogo wa kuwaokoa watu waliozama lakini pia bodi vibaya.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana