Pata taarifa kuu
TANZANIA-KOROSHO-JOHN MAGUFULI

Rais Magufuli:Serikali itanunua korosho kwa bei ya 3300 kwa kilo

Serikali ya Tanzania imekata mzizi wa fitina kwa kuamua kununua korosho kwa bei ya 3300 kwa kilo.

Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais wa Tanzania, John Magufuli afrinews.com
Matangazo ya kibiashara

Rais John Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu Mjini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri aliowateua baada ya kufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.

Zaidi ya tani za korosho laki mbili zilizalishwa nchini Tanzania mwaka huu.

Awali, sakata la korosho lilizua gumzo nchini Tanzania baada ya bodi ya korosho kuarifu kuwa bei elekezi itakuwa 1500 kwa kilo, suala lililozua mvutano baina ya makundi mbalimbali katika jamii.

Rais Magufuli ameliagiza Jeshi la wananchi wa Jeshi la Wananchi wa tanzania kuhakikisha korosho inasafirishwa kutoka mikoa inayozalisha zao hilo na kuhifadhiwa kwenye maghala maalumu.

"Viongozi wa jeshi mjipange kuhakikisha suala hili linaanza mara moja,"amesema Rais Magufuli, aliyekuwa akizungumza kwa msisitizo.

Aidha kiongozi huyo wa nchi ametaka benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kusimamia mchakato wa ununuaji korosho kutoka kwa wakulima na kuhakikisha hakuna mkulima anayepunjwa jasho lake.

"TADB hakikisheni mnasimamia kikamilifu, mkulima alipwe fedha zake zote,"

Zao la korosho hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na ni mojawapo ya mazao yanayoliingizia taifa la Tanzania fedha nyingi za kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.