Pata taarifa kuu
TANZANIA-SAMIA SULUHU-AFYA

Akina mama 30 hupoteza maisha kila siku kutokana na changamoto za uzazi nchini Tanzania

Serikali ya Tanzania imezindua kampeni maalumu ya kukabiliana na changamoto za kiafya kwa akina mama wakati wa kujifungua.

Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Makamu wa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Tanzania/VPO
Matangazo ya kibiashara

Kampeni hiyo iliyopewa jina la  "Jiongeze, tuwavushe salama" imezinduliwa Mkoani Dodoma na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu huku ripoti kadhaa za afya zikionyesha uwepo wa vifo vya akina mama wakati wa kujifungua.

Uzinduzi wa kampeni hii unakuja wakti ikikadiriwa kuwa wanawake 11, 000 sawa na wanawake 30 kila siku hupoteza maisha kila mwaka kutokana na changamoto za uzazi, ripoti ya Wizara ya Afya ya mwaka 2017 imeainishwa.

Aidha ripoti zinasema ni asilimia 40 tu ya wanawake wajawazito wanaohudhuria kliniki wakatti wa ujauzito.

Kampeni iliyozinduliwa inalenga kuongeza msukumo kwa serikali na wadau wengine wa afya kuongeza uwajibikaji ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi wa watoto wachanga.

Raia wengi wa Tanzania husihi maeneo ya vijijini ambako bado huduma za afya si za kuridhisha.

Sikiliza ripoti ya Mwandishi wa RFI Kiswhaili, Sabina Mpelo kupitia kiunganishi hapo juu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.