Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Ofisi ya Mashitaka yaomba kifungo cha miaka 22 dhidi ya Diane Rwigara

media Diane Rwigara mkosoaji mkubwa wa Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS/Jean Bizimana

Kesi ya mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara na mama yake imesikilizwa Jumatano wiki hii katika mahakama ya Kigali. Baada ya kuzuiliwa jela kwa muda wa mwaka, wawili hawa, waliaochiliwa kwa dhamana mapema mwezi Oktoba, waliwasili mahakamani bila kusindikizwa na polisi.

Kesi hiyo ilimalizika baada ya saa tano. Upande wa mashtaka, umeomba kifungo cha miaka 15 dhidi ya Diane Rwigara kwa madai ya kuchochoea uasi na miaka 7 kwa madai ya kughushi stakabadhi katika kujaribu kuwania uchaguzi wa urais mnamo mwezi Agosti 2017.

Mama yake ameombwa kufungwa miaka 22 kwa madai ya "kuchochea uasi" na "kuchochea mgawanyiko" nchini Rwanda kwa mawasiliano kupitia Whatsapp na wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni nje ya nchi.

Upande wa utetezi umebaini kwamba upande wa mashitaka haukuonyesha ushahidi.

Watuhumiwa wote wawili wamekanusha shutma dhidi yao. Wanasheria wao wamesema hakuna ushahidi wowote kwa shutma dhidi ya wateja wao. Uamuzi utatolewa tarehe 6 Desemba. Ndugu wa familia ya Rwigara wameshtumu jinsi kesi hiyo ilivyoharakishwa. Hayo yanajiri wakati Diane Rwigara, siku ya Jumanne alitoa kauli kali dhidi ya utawala.

Katika siku za hivi karibuni Diane Rwigara ameonekana mkosoaji mkubwa dhidi ya utawala wa Kagame. "Muda si mrefu nimetoka jela," Diane Rwigara ameliambia shirika la Habari la AFP kabla ya kuongeza kuwa nchi yake "imekuwa kama gereza", ambapo "mlinzi (...) si mwengine bali ni chama tawala, RPF, ambacho kinatulazimisha kufanya jinsi kinavyotaka, na jinsi tunavyotakiwa kusema ".Amesema yuko tayari kurudi jela ili kutetea haki yake ya uhuru wa kujieleza.

Kwa upande wake shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Amnesty International limeomba shutma dhidi ya Diane Rwigara na mama yake zifutwe, huku likibaini kwamba kesi hiyo ni ya kisiasa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana