Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
E.A.C

Uganda yasimamisha shughulizi za ujenzi wa reli ya mwendo kasi

media Mji mkuu wa Uganda, Kampala. REUTERS/James Akena/File Photo

Uganda inasitisha ujenzi wa reli ya mwendo kasi kutoka jijini Kampala kwenda katika mpaka wa Kenya wa Malaba, hadi pale Kenya na China itakapotatua changamoto za kifedha.

Waziri wa fedha wa Uganda Matia Kasaija ameliambia Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Moniter kuwa, serikali yake imesitisha mradi huo baada ya kutopata hakikisho kutoka kwa Kenya na mfadhili wa mradi huo China, kuhusu ujenzi wa reli hiyo.

Badala yake, serikali ya Uganda inasema itakarabati reli yake ya zamani kuunganisha mataifa hayo jirani.

Hata hivyo, Kenya inaonekana kutotishwa na hatua hiyo ya Uganda baada ya Waziri wa Uchukuzi James Macharia kusema kuwa, kwa sasa serikali hiyo inaimarisha Bandari ya Kisumu ili kurahihisha usafirishaji wa mizigo kupitia Ziwa Victoria kwenda Uganda na Rwanda.

Baada ya kumaliza reli ya kisasa kutoka mjii wa Pwani wa Mombasa kwenda jiji kuu la Nairobi, Kenya inaendelea na ujenzi wa reli hiyo kutoka Nairobi kwenda Naivasha, na baadaye kutoka Naivasha kwenda Kisumu.

Mataifa hayo mawili yalikuwa yamekubaliana kuwa, ujenzi wa reli kutoka Kampala kwenda Malaba itaanza baada ya ujenzi wa mradi kutoka Nairobi kwenda Naivasha kukamilika, lakini mradi huo wa Dola Bilioni 2.3 sasa, haifahamiki utaanza lini.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana