Pata taarifa kuu
TANZANIA-UN-HAKI ZA WANAWAKE

Mwanaharakati Rebeca Gyumi atunukiwa tuzo na Umoja wa Mataifa

Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi ametunukiwa tuzo ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018.

Mwanaharakati mtetezi wa haki za watoto na wanawake nchini Tanzania, Rebeca Gyumi
Mwanaharakati mtetezi wa haki za watoto na wanawake nchini Tanzania, Rebeca Gyumi Daily News
Matangazo ya kibiashara

Gyumi ni mwanaharakati wa muda mrefu nchini Tanzania ambaye hasa amekuwa  akijishughulisha kutetea haki za wanawake na watoto na ameshinda tuzo hiyo sanjari na wenzake watatu.

Tangazo la ushindi wake lililotolewa kupitia mtandao wa Twitter na Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa, Maria Fernanda Espinosa ambaye pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa harakati zao za kusukuma mbele haki za binadamu.

Washindi wengine ni Asma Jahangir mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Pakistan ambaye alipoteza maisha mwaka huu.

Halfa ya utoaji wa tuzo hiyo ambayo kihistoria ilianza kutolewa mwaka 1973,  itafanyika Disemba 10 nchini Marekani.

Katika harakati zake,mwaka 2016 Gyumi alishinda kesi ya kihistoria ya kupinga sheria ya ndoa ya mwaka 1971 nchini Tanzania ambayo inaruhusu wasichana wenye umri wa miaka 14 kuolewa

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rebeca Gyumi alitumia fursa ya ushindi wake kuwashukuru watanzania ambao walimiminika mtandaoni kumpongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.