Biashara ya samaki yadorora katika soko la Kimataifa la Ferry Jijini Dar es Salaam
Wafanyabiashara wa samaki katika soko la samaki la Kimataifa la Ferry Jijini Dar es Salaam wameelezea kusuasua kwa biashara zao siku chache baada ya kuripotiwa mabadiliko ya hali ya hewa na viuashiria vya mvua.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mwandishi wetu Fredrick Nwaka mapema leo alifika sokoni hapo na kuzungumza na wachuuzi na watumiaji wa kitoweo hicho ambao wengi wamekiri bei ya kitoweo hicho imeongezeka maradufu.
"Bei ya samaki imeongezeka sana, jambo linalotupatia wakati mgumu sisi wachuuzi kukuza biashara zetu,"alieleza mchuuzo mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Seif Hamis
Soko la samaki la Ferry hutegemewa na wafanyabiashara wengi katika Jiji la Dar es salaam na hata nje ya nchi. Mara kadhaa serikali ya Tanzania imechukua hatua za kuhakikisha soko hilo linakidhi viwango vya kimataifa kwa kuhudimia wakazi wa ndani na nje ya nchi.
Mapema wiki hii, Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, TMA ilitoa tangazo ikionya wavuvi kutoingia baharini kutokana na upepo mkali.
Ni kilio cha hali ngumu ya biashara katika soko la kimataifa la samaki la Ferry Jijini Dar es Salaam. Hapa wachuuzi wa samaki wanapiga moyo konde licha ya hali ngumu ya biashara.
Mwajuma yo ni Ofisa Uvuvi na Kaimu Mwenyekiti wa Soko la Samaki la Ferry amesema licha ya hali ya kibiashara kuwa tete lakini usalama ni suala la muhimu kwa watumiaji wote wa soko hilo wakiwemo wavuvi.
Fuatilia matangazo yetu ya jioni saa 12 Jioni ili kupata undani wa taarifa hii na nyinginezo