Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mohamed Dewji apatikana siku 10 baada ya kutekwa

media Mohamed Dewji youtube

Mfanyabiashara tajiri kijana nchini Tanzania aliekuwa ametekwa sasa ni zaidi ya juma moja, hatimae amapatikana. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kamishna msaidizi muandamizi wa jeshi la Polisi ambae pia ni kamanda wa kanda maalum ya polisi Dar es salaam Lazaro Mambo Sasa, amesema wahalifu walimkwenda kumtelekeza Mfanyanabiashara huyo maeneo ya Gymkana jijini Dar es salaam na gari walilotumia wakati wa kumteka siku 10 zilizopita.

Kamishna msaidizi muandamizi wa jeshi la Polisi ambae pia ni kamanda wa kanda maalum ya polisi Dar es salaam Lazaro Mambo Sasa amewambia waandishi wa habari kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likifuatilia tukio hilo la utekaji lisilokuwa la kawaida.

Na kwamba usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi majira ya saa nane kwenda tisa wailipokea ripoti kwamba Mohamed Dewji amepatikana akiwa hai na salama. Wahalifu walikwenda kumtupa eneo la Gymkhana.

Jeshi la Polisi limekwenda kuthibitisha na kumuona akiwa mwenye afya njema licha ya kuonekana kuwa mwenye uchovu.

Lazaro Mambo sasa amesema kulingana na taarifa za hapo awali kwamba waliomteka Mo sio raia wa Tanzania, zimethibitishwa na Mo mwenyewe ambae amesema wahalifu walikuwa wanatumia lugha inayofanana na lugha inayotumiwa huko nchini Afrika Kusini.

Mohamed Dewji ameonekana mwenye uchovu ameonge kwa unyonge na kutowa shukrani za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa rais John P Magufuli na Watanzania wote.

Kabla ya hapo aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wa kampuni ya Mohamed Dewji Interprises akiwashkuru Watanzania, na kwamba amerejea nyumbani salama.

Awali msemaji wa Familia Azim Dewji alisikika akieleza mazingira ya kupatikana kwa Mo ambapo amesema walipokea simu majira ya saa nane na nusu kuelekea saa nane na dakika 40 Mo akiwafahamisha kuwa yupo mzima eneo la Gymkhana, familia haikuamini, wakaelekea eneo la tukio na kumkuta kweli akiwa salama.

Aidha familia imesema imemkuta akiwa hajafungwa kamba.

Mohamed Dewji Aalitekwa alfajiri ya Octoba 11 wakati akielekea kufanya mazoezi katika Hoteli ya Colissium jijini Dar eslaam.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana