Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
E.A.C

Rais Kagame amteua Waziri mpya wa Mambo ya nje na Ulinzi

media Raisi wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Ruben Sprich

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amemteua Waziri mpya wa Mambo ya nje na Ulinzi katika mabadiliko ya hivi punde katika Baraza la Mawaziri.

Hatua hii ya rais Kagame imekuja, baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje Louise Mushikiwabo, kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa muungano wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, La Francophonie.

Rais Kagame amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na mwanadiplomasia wa siku nyingi Richard Sezibera, kuwa Waziri mpya wa Mambo ya nje.

Sezibera mwenye umri wa miaka 54, amerejea kwenye Baraza la Mawaziri baada ya awali kuwahi kuhudumu kama Waziri wa afya.

Aidha, Jenerali wa Jeshi Albert Murasira, kuwa Waziri mpya wa Ulinzi, anachukua nafasi ya James Kabarebe ambaye amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Kabarebe ambaye anaonekana na wachambuzi wa siasa kama mtu mwenye ushawishi kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, sasa atakuwa mshauri wa rais Kagame kuhusu masuala ya usalama.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana