Pata taarifa kuu
KENYA-UFISADI-MICHEZO

Hassan Wario akabiliwa na mashitaka ya ufujaji wa fedha katika Olimpiki Rio

Aliyekuwa Waziri wa Michezo nchini Kenya Hassan Wario amefikishwa Mahakamaji jijini Nairobi na kushatakiwa kwa madai ya ufisadi. Kwa miaka kadhaa wanariadha wa Kenya wanaoshinda medali katika michezo ya Olimpiki na ya Jumuiya ya Madola wamekua wanalalamika hawapati pesa kutoka Nike.

Aliye kuwa Waziri wa Michezo wa Kenya Hassan Wario katika mkutano na waandishi wa habari Nairobi, Mei 13, 2016.
Aliye kuwa Waziri wa Michezo wa Kenya Hassan Wario katika mkutano na waandishi wa habari Nairobi, Mei 13, 2016. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wario na maafisa wengine wa zamani katika Wizara ya Michezo na Kamati ya Michezo ya Olimpiki, wameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya Shilingi Milioni 55, zilizotolewa na serikali, kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil.

Pesa hizo inadaiwa zilikua ni tiketi za ndege za kikosi cha Kenya lakini maafisa walipandisha bei ya tiketi hizo kupita kiasi kwa manufaa yao wenyewe, kulingana na ripoti ya kamati ya kuchunguza kashfa hiyo.

Wario alikwenda kujisalimisha kwa Polisi siku ya Alhamisi, na kukamatwa.

Noordin Haji, Mkuu wa Mashtaka ya Umma nchini humo anasema ana ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashataka wawili hao na maafisa wengine wa zamani waliohudumu katika Wizara ya Michezo.

Waziri huyo wa zamani wa Michezo, siku hizi ni Balozi wa Kenya nchini Austria.

Wengine watakaochunguzwa ni mwenyekiti wa zamani wa chama cha Olimpiki cha Kenya na mkimbiaji hodari Kipchoge Keino, katibu wa zamani wa wizara inayosimamia michezo Richard Titus Ekai, mkurugenzi wa zamani wa usimamizi katika wizara hiyo Harun Komen, kiongozi wa kikosi cha Kenya katika michezo ya Olimpiki ya Rio Stephen arap Soi, Patrick Kimathi na katibu wa cha Olimpiki cha Kenya Francis Kinyili Paul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.