Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Nchi nne za Jumuiya ya Afrika Mashariki zakabiliwa na kitisho cha ugonjwa wa Ebola

media Maafisa wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamevaa nguo zinazowakinga na maambukizi ya virusi vya Ebola wakati mafunzo ya kukabiliana dhidi Ebola karibu na mji wa Beni, Kivu Kaskazini. REUTERS/Samuel Mambo/File Photo

Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi zimetakiwa kuchukua tahadhari ya haraka kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola, kwa sababu hali inaweza kubadilika wakati wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO).

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema hatari ni kubwa kwa Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini na tayari nchi hizo zimeambiwa kuchukuwa hatua za haraka ili kuzuia ugonjwa huo.

Kauli hii inakuja baada ya mkutano maalumu wa dharura uliofanyika mjini Geneva kujadili hali ya ugonjwa huu nchini DRC.

Burundi na Sudan kusini ni nchi mbili za Afrika Mashariki ambazo zinaonekana kuwa katika hatari zaidi kutokana na kuingia na kutoka kwa watu mpakani kutoka nchi za DRC, Rwanda na Uganda.

Wizara ya afya nchini Burundi imeeleza kwamba tayari kuna vifaa vya kukabiliana na janga iwapo litatokea.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC bado hauhitaji jitihada za dharura za kimataifa huku likisisitiza kuwa linafuatilia kwa karibu ugonjwa huo.

Kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mzozo unaoendelea, Kupoteza imani kwa jamii katika maeneo yalioathirika, yote haya yanatatiza jitihada za kudhibiti ugonjwa huo.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DR, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.

Mapigano katika eneo hilo yanafanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo.

Kwa sasa tahadhari imetolewa kwa wananchi kutosafiri kwenda katika maeneo yalioathirika na kuripoti dalili zozote wanazozishuku.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana