Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Bobi Wine aishtumu polisi kutumiwa kisiasa

media Mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, anayejulikana kwa jina la Bobi Wine kupitia muziki wa Pop, afanya mkutano na waandishi wa habari huko Washington, DC, Septemba 6, 2018. © AFP

Mbunge wa upinzani ambaye pia ni Mwanamuziki nchini Uganda Bobi Wine, amewashtumu Polisi kwa kuzuia tamasha aliloandaa mwishoni mwa juma hili jijini Kampala.

Polisi wanasema wameamua kusitisha tamasha hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika katika uwanja wa Michezo wa Naambole kwa sababu, hajafanya maandalizi ya kutosha na wasimamizi wa uwanja huo.

Hata hivyo, mbunge huyo ambaye amejipatia umarufu siku za hivi karibuni, na kuoneakana kupendwa na vijana wengi nchini humo, amesema serikali inahofia ushawishi wake hasa kwa vijana.

Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.

Bobi Wine alitarajia kutumia tamasha hilo kuzindua album yake mpya inyofahamika kama Kyarenga.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana