Pata taarifa kuu
TANZANIA-DEWJI-USALAMA

Zawadi nono yatolewa kwa atakayewezesha kupatikana kwa Mohammed Dewji

Familia ya bilionia wa Tanzania, Mohammed Dewji, anayefahamika kwa jina la Mo Dewji imetoa kitita cha karibu dola nusu milioni kwa atakayetoa taarifa ya kupatikana kwa tajiri huyo kijana barani Afrika.

Bilionia wa Tanzania Mohammed Dewji katika ofisi yake Dar es Salaam, Aprili 23, 2015.
Bilionia wa Tanzania Mohammed Dewji katika ofisi yake Dar es Salaam, Aprili 23, 2015. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Familia inatoa zawadi nono ya shilingi za Tanzania bilioni moja( sawa na dola 437,000) kwa mtu yeyote ambaye atatoa taarifa ya kusaidia kupatatikana kwa Mohammed Dewji," amesema Azim Dewji, msemaji wa familia, katika mkutano na waandishi wa habari huko Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Mo Dewji, mwenye umri wa miaka 43, ni billionaire mdogo zaidi katika bara la Afrika. Alitekwa nyara Oktoba 11, mapema asubuhi, alipokuwa akiingia kwenye ukumbi wa michezo kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa kiuchumi nchini Tanzania, Dar es Salaam.

Polisi ilizindua operesheni ya kumtafuta bilionea huyo na sehemu anakofichwa. Kwa mujibu wa mamlaka ya Tanzania, watu zaidi ya ishirini tayari wamekamatwa kuhusiana na uchunguzi.

Mo Dewji ni Mkurugenzi Mkuu na mmiliki wa kampuni ya METL, inayopatikana katika nchi kadhaa katika nyanja ya kilimo, bima, usafiri, vifaa au biashara ya kilimo.

Alizaliwa Tanzania, alisoma Chuo Kikuu cha Georgetown huko Marekani. Mwaka wa 2013, alikuwa Mtanzania wa kwanza kupiga fora katika gazeti la Forbes, na mwaka 2015 alitangazwa na Forbes kitengo cha Afrika kama "Mtu anayeongoza kwa utajiri" mwaka huo. Kwa mujibu wa gazeti hilo, Mo Dewji anashikilia nafasi ya 17 kwenye orodha ya mabilionea wa Kiafrika ambaye anakadiriwa kumiliki dola bilioni 1.54 (sawa na euro bilioni 1.29).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.