Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-USALAMA

Uhuru Kenyatta: Wanajeshi wa Kenya watasalia Somalia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema, jeshi la nchi hiyo litaendelea kusalia nchini Somalia chini ya mwavuli wa jeshi la Umoja wa Afrika AMISOM, hadi pale usalama na amani vitavyorejea katika taifa hilo.

Helikopta ya jeshi la Kenya ikijiandaa kusafirisha miili ya watu saba waliouawa katika mashambulizi ya Al Shabab kaskazini mwa Kenya karibu na mji wa Wajir Januari 12, 2012.
Helikopta ya jeshi la Kenya ikijiandaa kusafirisha miili ya watu saba waliouawa katika mashambulizi ya Al Shabab kaskazini mwa Kenya karibu na mji wa Wajir Januari 12, 2012. REUTERS/Charles Makunda
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ameongeza kuwa, makundi ya kigaidi yameendelea kuwa, tishio kwa nchi za ukanda wa pembe ya Afrika kwa kuwashambulia na kuwatisha raia.

Jeshi la Kenya liliingia nchini Somalia mwaka 2011, baada ya  magaidi wa Al Shabab kuanza kuwateka watalii katika mpaka wa nchi hiyo katika operesheni iliyopewa linda nchi, kabla ya baada kujiunga na jeshi la Umoja wa Afrika.

Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somalia mwaka wa 2011 kutokomeza kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Kwa sasa jeshi la Kenya linahudumu chini ya jeshi la muungano wa afrika AMISOM, ambalo linaunga mkono serikali ya sasa ya somalia.

Wapiganaji wa Al shabaab wameimarisha operesheni zao nchini Kenya, na hivyo kuwa pigo kubwa kwa mipango ya Kenya ya kuwatuma wanajeshi wake katika maeneo ya mipakani kuzuia wapiganaji wa kundi hilo kuingia nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.