Pata taarifa kuu
KENYA-MAUAJI-MWANAHABARI-MAHAKAMA

Mwanahabari na mpenzi wake wakanusha madai ya kumuua mfanyibiashara

Mwanahabari nchini Kenya Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu maarufu kama Jowie, wamekanusha mashtaka ya kutekeleza mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani, wiki kadhaa zilizopita jijini Nairobi.

Mwanahabari Jacque Maribe (Kushoto) akiwa na mpenzi wake Joseph Irungu wakiwa Mahakamani jijini Nairobi Oktoba 15 2018, walipokuwa Mahakamani jijini Nairobi
Mwanahabari Jacque Maribe (Kushoto) akiwa na mpenzi wake Joseph Irungu wakiwa Mahakamani jijini Nairobi Oktoba 15 2018, walipokuwa Mahakamani jijini Nairobi nairobinews.nation.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wamemwambia Jaji Jessie Lessit, kuwa wanafahamu mashtaka dhidi yao lakini, hawakuhusika kama upande wa mashtaka unavyodai.

Hatua hii imekuja, baada ya Mwanahabari huyo wa Televisheni ya Citizen kupimwa akili na mpenzi kupata huduma za afya baada ya kujeruhiwa begani baada ya kudaiwa kupigwa risasi.

Mahakama imeamua kuwa watasalia kizuizini hadi siku ya Jumatano wiki hii, wakati kesi itakapotajwa.

Wameomba kuachiliwa huru kwa dhamana lakini, Mahakama inayosikiliza kesi hii imesema, ombi hilo liwasilishwe katika Mahakama nyingine.

Kesi hii imevutia hisia kubwa nchini Kenya kutokana namna mfanyibiashara huyo alivyouawa kwa kukatwa shingo, na wanaodaiwa kuhusika akiwemo mwanahabari huyo maarufu.

Mfanyibiashara huyo aliuawa baada ya kurejea Nairobi, akitokea Juba Sudan Kusini, anakoaminiwa kuishi na kufanya kazi.

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, Maribe alimsaidia mpenzi wake kutekeleza mauaji hayo, kwa kumficha huku baadhi ya vitu vilivyotumiwa kama kisu, vikipatikana nyumbani kwake.

Iwapo wawili hao watapatikana na hatia, watahukumiwa maisha jela kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.