Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 16/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Mwanahabari na mchumba wake waendelea kuzuiwa kwa madai ya mauaji

media Jacque Maribe (Kushoto) akiwa na mpenzi wake Joseph Irungu (Kulia) washukiwa wa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, wakiwa Mahakamani Oktoba 09 2018 jijini Nairobi NationBreaking

Mahakama Kuu jijini Nairobi nchini Kenya imeagiza kuendelea kuzuiwa kwa washukiwa wawili wa mauaji ya mwanadada Monica Kimani, aliyepatikana ameuawa nyumbani kwake mwezi Septemba.

Viongozi wa Mashtaka, wamesema watamfungulia kesi ya mauaji Mwanabahari maarufu nchini humo Jacque Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu ambaye ndio mshukiwa mkuu.

Jaji Jessi Lessit amesema wawili hao watazuiwa hadi siku ya Jumatatu wiki ijayo, na kuagiza kuwa Bi. Maribe afanyiwe uchunguzi wa kiakili katika Hospitali ya wagonjwa wa akili kabla ya kujibu mashtaka yanayomkabili.

Irungu naye ametakiwa kupewa huduma ya matibabu baada ya kupata jeraha la bega. Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanadai kuwa mshukiwa huyo alijipiga risasi mwenyewe wala hakushambuliwa.

Kiongozi wa Mashtaka Noordin Haji, ameagiza wawili hao kufunguliwa kesi ya mauaji kwa madai kuwa walishirikiana kumuua mwanadada huyo.

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana