Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/10 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/10 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Waalimu watishia kuanza mgomo Oktoba 17 Kenya

media L'école du village d'Umoja au Kenya Shule ya Umoja nchini Kenya (Photo : Méryl Bécède)

Chama cha Walimu nchini Kenya KNUT, kimetangaza kuwa kutakuwa mgomo wa walimu nchini humo kuanzia tarehe 17 mwezi huu, iwapo Tume ya kuwaajiri Walimu haitaachanana sera ambazo chama hicho kinasema zinatekelezwa bila ya kuwepo mashauriano.

Katibu Mkuu wa chama hich Wilson Sossion amesema, iwapo tume hiyo itaendelea na sera hizo ambazo ni pamoja na kuwahamisha Walimu wakuu, mgomo huo utaendelea hadi pale suluhu itakapopatikana.

Iwapo mgomo utafanyika, utaathiri mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne na darasa la nane, unaotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.

Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion amesema TSC haijaahidi kuyashughulikia malalamiko wanayoibua. KNUT inaitaka TSC kuwapandisha vyeo walimu, kuistisha mpango wa kuwahamisha walimu unaoendelea, vile vile shughuli ya kutathimini utendakazi wao.

Mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu chama cha walimu nchini KNUT kiliahirisha mpango wake wa mgomo uliokuwa ulipangwa kuanza tarehe 1 Septemba wakati wakiendeleza mazungumzo na muajiri wao TSC.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana