Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-KISWAHILI-AFRIKA KUSINI

Dokta Kamfipo Gidion: Wasomi wachangamkie fursa ya kufundisha lugha ya Kiswahili

Wasomi wa taaluma ya Kiswahili wametakiwa kutumia fursa ya baadhi ya mataifa kurasimisha lugha hiyo, kutafuta fursa za kufundisha lugha ya Kiswahili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dokta Kamfipo Gidion akihojiwa na RFI Kiswahili Oktoba 4, 2018
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dokta Kamfipo Gidion akihojiwa na RFI Kiswahili Oktoba 4, 2018 RFI Kiswahili/Fredrick Nwaka
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni nchini ya Afrika Kusini ilitangaza kurasimisha Kiswahili katika ngazi ya msingi nchini humo.

Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Elimu ya Msingi nchini Afrika Kusini Angie Motshekga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Daktari Gideon Kamfipo ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya RFI kwamba licha ya Afrika Kusini kutokuwa nchi ya kwanza kurasimisha Kiswahili, wasomi wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.

"Sisi lazima tujithamini, kama Afrika Kusini iinatambua Kiswahili sisi lazima tuonyeshe kukithamini na kukienzi,"ameeleza Daktari Kamfipo.

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa zaidi katika nchi za Tanzania na Kenya na pia huzungumzwa kiasi katika mataifa zaidi ya 11 barani Afrika.

Baadhi ya mataifa hayo ni Burundi, Uganda, Msumbiji, Zambia, MalawiSudani Kusini, DRC, Somalia na Rwanda.

Sikiliza habari hii kwenye kiunganishi hapo juu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.