Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Mjadala kuhusu kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa mwaka 2022 waanza Kenya

Mjadala wa kuibadilisha Katiba ya Kenya, lengo likiwa ni kubadilisha mfumo wa uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022, umeanza tena.

Viongozi wa upinzani nchini Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat, Januari 11 Nairobi.
Viongozi wa upinzani nchini Kenya Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat, Januari 11 Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na vinara wao Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanashinikiza, mabadiliko hayo kufanyika, huku wakitaka kuwe na Waziri Mkuu mwenye mamlaka na kuondoa wadhifa wa rais.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na William Ruto Naibu rais na wengine kutoka chama tawala wanaona hakuna haja ya hilo kufanyika.

Wakati huo huo, Naibu rais Ruto, amemshtumu kiongozi wa upinzani ambaye ni Raila Odinga kwa kutaka kumwondoa katika chama tawala cha Jubilee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.