sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Watu kadhaa wafariki baada ya kivuko cha MV kuzama Mwanza

media Kivuko MV Nyerere chazama Ziwa Victoria Youtube.com

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho, kwa mujibu wa mtandao wa kijamii maarufu zaidi nchini Tanzania, Jamii Forum.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.

“Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka”, amesema Mkuu wa Polisi mkoani Mwanza, kulingana na taarifa zilizokusanywa na Jamii Forum.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 19 tarehe 1 Julai 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika zinasema watu wengi wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Hata hivyo gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa watu sita wamefariki dunia na wengine 20 wameokolewa.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana