Pata taarifa kuu
KENYA-IMF-UCHUMI

Wabunge kupigia kura mapendekezo ya rais Kenyatta kuhusu ushuru mpya wa mafuta

Wabunge nchini Kenya leo Alhamisi mchana, watajadili na kupigia kura mapendekezo ya rais Uhuru Kenyatta kuhusu ushuru mpya uliowekewa bei ya mafuta, suala ambalo limewagawa wabunge wa chama tawala na upinzani.

Mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

jadala huu, unakuja siku chache baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangaza kupunguzwa kwa utozwaji ushuru kwa bidhaa hiyo muhimu kutoka asilimia 16 hadi asilimia nane.

Hatua huu ilikuja, baada ya Wakenya kulalamika kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta kutokana na ongezo hilo la ushuru.

Jana, rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga waliwakutana na wabunge wao na kuwahimiza kuunga mkono mabadiliko hayo.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge kutoka chama tawala na upinzani wamesema hawataunga mkono mapendekezo hayo kwa sababu hawaoni kama yataleta unafuu kwa wananchi wa kawaida, iwapo ushuru huo hautaondolewa.

Iwapo mapendekezo hayo yatapishwa, kiwango cha ushuru kitapungua kwa asilimia hamsini, punguzo ambalo raia wa kawaida wanaona kuwa, bado halina msaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.