Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-HAKI-USALAMA

Rais Kagame amuonya Ingabire kutuliza msimamo wake

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewaonya wale wote wanaosema kuwa hatuwa ya hivi karibuni ya kuwaacha huru wafungwa imekuja kutokana na shinikizo kutoka katika mataifa ya magharibi.

Rais Paul Kagame hakufurahia taarifa za Victoire Ingabire tangu alipochiliwa kutoka gerezani.
Rais Paul Kagame hakufurahia taarifa za Victoire Ingabire tangu alipochiliwa kutoka gerezani. © Madoka Ikegami/POOL Via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Kagame bila kutaja jina lake amemuonya Victoire Ingabire kiongozi wa upinzani wa chama cha FDU ambae aliachiwa huru hivi karibuni kupitia msamaha wa rais na kueleza kwamba hakuomba msamaha wa kutaka aachiwe huru.

Rais Paul Kagame amesema hakuna anayeweza kumshinikiza.

Akihotubia bunge baada ya wabunge waliochaguliwa hivi karibuni kuapishwa rasmi, rais Kagame amesema msamaha aliotoa “ndiyo njia” aliyochagua ya kutatua matatizo na kujenga taifa hla Rwanda.

Victoire Ingabire, kiongozi wa chama cha FDU, ameahidi kuendelea na mapambano yake ya demokrasia nchini Rwanda.

Victoire Ingabire alipotoka gerezani alimshukuru rais Kagame kwa msamaha wake lakini akasisitiza kuwa hakuomba msamaha kwa kuwa hakufanya kosa lolote.

Bi Ingabire , ambaye ni kutoka kabila la wahutu, alikamatwa na kufungwa baada ya kuhoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Rwanda ya 1994 hayakuhusisha watu wa kabila la Wahutu. Alishtumiwa kuchochea chuki na kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, kabila la rais Paul Kagame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.