Pata taarifa kuu
RWANDA-PAUL KAGAME-SIASA

Victoire Ingabire:Niko tayari kusaidia maendeleo ya Rwanda

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire Umuhoza ameseema yuko tayari kusaidaia maendeleo ya nchi ya Rwanda siku chache baada ya kuachiliwa huru.

Mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire Umuhoza na mwanamuzi Kizito Mihigo baada ya kuachiliwa huru katika gereza la Nyarugenge nchini Rwanda
Mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire Umuhoza na mwanamuzi Kizito Mihigo baada ya kuachiliwa huru katika gereza la Nyarugenge nchini Rwanda www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Ingabire, mwanamuziki Kizito Mihigo ni miongoni mwa wafungwa zaidi ya 2000 walioachiliwa huru kwa msamaha wa rais Paul Kagame. Walihukumiwa kwa nyakati tofauti na walikuwa wakitumikia vifungo vyao katika gereza la Nyarugenge.

"Nina furaha kwa hatua iliyochukuliwa na rais na sasa nitarejea kuendelea na maisha kama kawaida na kusaidia maendeleo ya nchi,"amesema Ingabire, akinukuliwa na gazeti la The New Times la Rwanda.

Ingabire ni kiongozi wa chama cha upinzani cha United Democratic Forces of Rwanda (FDU-Inkingi) na alihukumiwa kwenda jela kifungo cha miaka 15, miaka minane iliyopita.

Tangu wakati huo ulimwengu umekuwa ukipaza sauti kuachiliwa kwake na hatua ya serikali ya Rwanda kumuachilia huru inatajwa kuwa hatua muhimu kuchukuliwa na utawala wa rais Paul Kagame ambaye anaongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa muhula wa tatu sasa.

Mwanaharakati mwingine aliyeachiliwa huru ni mwanamuzi Kizito Mihigo ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuratibu njama za mauaji ya rais Paul Kagame.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.