Pata taarifa kuu
Rwanda - Sheria

Paul Kagame awasamehe wafungwa 2140

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewaachia huru wafungwa 2140 walioomba msamaha, na ambao walikuwa wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali ya uhalifu. Mara baada ya kuachiwa huru Ingabire amesema huenda sasa ikawa ndio mwanzo wa uhuru wa kisiasa nchini Rwanda.

Victoire Ingabire akijadiliana na wakili wake Iain Edwards, Mars 25 2013  Kigali.
Victoire Ingabire akijadiliana na wakili wake Iain Edwards, Mars 25 2013 Kigali. AFP PHOTO / Stephanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Jumla ni wafungwa 2.140 kutoka katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo laini wengi wakiwa ni kutoka katika mkoa wa Huye.

Miongoni mwao ni Victoire Ingabire mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FDI, Force Democratique Unies du Rwanda ambae alikuwa amehukumiwa tangu mwaka 2010, pamoja na mwanamuziki Kizito Mihigo ambae alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

Ingabire alifungwa mwaka 2010, alipatikana na hatia ya kuchochea raia kuiasi serikali, kuunda makundi ya silaha ili kuivuruga nchi na kupuuza mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi.

Mnamo Februari 2015, Kizito Mihigo alihukumiwa miaka 10 gerezani baada yakukiri kuhusika na uhalifu, ikiwa ni pamoja na njama ya kumuuwa Rais Paul Kagame na viongozi wengine wa nchi.

Upande wake Eugene Ndahayo makam mwenyekiti wa zamani wa chama cha FDI mbali na kupongeza anaona kuwa huenda hatuwa hii imekuja kutokana na shinikio inayoendelea kimataifa hasa wakati huu waziri wa mambo ya nnje wa sasa wa Mushikiwabo anawania nafasi yakuwa katibu mkuu wa shirika la nchi zinazo zungumza lugha ya Kifaransa.

Hata hivyo katibu mkuu wa serikali ya Rwanda anaehusika na mambo ya nnje, Olivier Nduhungirehe amesema hatuwa hiyo imekuja kutokana na ombi la wahusika wenyewe kumuandikia rais mara kadhaa wakimuomba msamaha na sio vinginevyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.