Pata taarifa kuu
KENYA-IMF-UCHUMI

Kodi mpya ya mafuta yazua upinzani mkubwa Kenya

Mgogoro katika sekta ya mafuta unaendelea nchini Kenya. Tangu Septemba 1, serikali imeweka kodi ya asilimia 16 kwa mafuta, na kusababisha hasira kubwa na upinzani kwa raia, huku bei za bidhaa mbalimbali zikipanda mara dufu.

Foleni kubwa ya magari Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Foleni kubwa ya magari Nairobi, mji mkuu wa Kenya. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Mahakama iliamuru taasisi husika kufuta kodi hiyo, lakini uamuzi huo umepuuziwa mbali. Wapinzani wa kodi hiyo wanaendelea kuonesha hasira yao.

Rais Uhuru Kenyatta anakabiliwa na upinzani mkubwa kufuatia hali hiyo. Kwa upande mmoja, anakabiliwa na shinikizo la kufuta kodi hii ambayo haiungwi mkono na wananchi wake. Kwa upande mwingine, kuna hatari ya kutokea uhasama mkubwa kati ya serikali yake na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambalo aliahidi kutekeleza kodi hii. IMF inaiomba Kenya kuongeza mapato yake ya kodi ili kulipa madeni.

Waangalizi wanaamini kwamba IMF inaweza kutishia kusimamisha mikopo ikiwa Kenya itafuta kodi yake. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya, Rais Kenyatta alikua anatarajiwa kuchukuwa hatua Jumanne wiki hii. Leo Jumatano, kwa hali yoyote, serikali yake itakuwa mbele ya mahakama.

Kufuatia malalamiko yaliyotolewa wiki iliyopita na wananchi kadhaa, Mahakama Kuu ya Kisumu iliamuru serikali kufuta ongezeko hili la asilimia 16. Lakini Tume ya Udhibiti wa Nishati, taasisi inayohusika na kusimamia sekta hiyo, ilikataa kutekeleza uamuzi huo wa mahakama, ikidai kuwa imepokea kopi tu ya hukumu, na wala sio ya nakala sahihi. Kutokana na hali hiyo waharakati waliwasilisha malalamiko mapya dhidi ya taasisi hiyo, wakiishtumu kudharau mahakama na kutotii amri ya mahakama. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa leo Jumatano.

Wakati huo huo shinikizo la kisiasa linaendelea kuongezeka. Chama kikuu cha upinznai cha ODM kimekosoa msimamo wa serikali wa kutotii amri ya mahakama na kuonyesha kuwa serikali imeshindwa kutetea maslahi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.