Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Sudan Kusini: Riek Machar akubali kutia saini mkataba wa amani

media Kiongozi wa waasi Riek Machar (kushoto) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakitia saini kwenye mkataba wa kugawana madaraka huko Khartoum, Sudan Agosti 5, 2018. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar hatimaye amekubali kutia saini mkataba wa amani na serikali. Tangazo hilo lilitolewa Alhamisi, Agosti 30 huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan, nchi ambayo inasimamia usuluhishi.

Mkataba wa amani ulikuwa tayari umeidhinishwa na serikali ya Sudan Kusini. Mkataba huu utasaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya watu wengi nchini humo tangu mwaka 2013.

Hatimaye upatanishi wa serikali ya Khartoum umezaa matunda. Kutokana na hatua hii ya Riek Machar kutia saini mkataba wa amani ambao serikali ya Sudan Kusini ilikua tayari imesahihisha, mchakato wa amani umezinduliwa upya. Lakini kunatakiwa jitihada ziongezwe mara dufu.

→ Soma zaidi: Riek Machar akataa kusaini mkataba wa amani Sudan Kusini

Siku ya Jumanne, Riek Machar alikataa kutia saini mktaba huo wa amani. Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini na makundi mengine ya upinzani walidai kuwa hoja zao ziingizwe katika nakala hiyo ya mwisho kabla ya kusainiwa mkataba wa amani. Hoja ambayo Riek Machar baadaye aliachana nayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Al Dir Diri Ahmed amesema.

Kwa mujibu wa Bw Diri Ahmed, hatua ya kutia saini ya mwisho kwenye mkataba huo itakua katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Afrika Mashauki (Igad). Tarehe ya mkutano huu itatangazwa hivi karibuni, amesema.

Hatua hii ni matokeo ya wiki kadhaa za mazungumzo katika nchi jirani ya Sudan. Mazungumzo haya yalipelekea kusainiwa mnamo mwezi Julai na mapema mwezi Agosti makubaliano kati ya Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar. Wanapanga kusitisha mapigano ya kudumu na kugawana madaraka katika nchi hii ndogo duniani.

Sudan Kusini, iliyopata uhuru wake kutoka Sudan tangu mwaka 2011, iliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe miaka miwili baadaye. Maelfu ya watu wameuawa na karibu milioni nne waliyahama makazi yao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana