Pata taarifa kuu
KENYA-MAREKANI-USHIRIKIANO-UCHUMI

Kenya na Marekani zakubaliana mikataba ya dola Milioni 900

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na mwenyeji wake rais wa Marekani Donald Trump mjini Washington na kuzungumzia masuala mbalimbali, ikwa ni pamoja na biashara na usalama.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta. Uhuru Kenyatta/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Rais Trump alisema Kenya na Marekani zitaendelea kushirikiana kuimarisha ushirikiano wao katika biashara, uekezaji na usalama.

Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema Kenya imekua na ushirikiano mzuri na wa kipekee na Marekani katika masuala ya usalama na ulinzi, hasa katika harakati za kukabiliana na ugaidi.

“Muhimu zaidi tuko hapa kuboresha ushirikiano wetu katika biashara na uekezaji, " alisema Rais Kenyatta.

Kwa upande mwengine Rais Uhuru Kenyatta ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba amefanikisha makubaliano yenye thamani ya mamilioni ya dola na Wawekezaji wa Kimarekani.

Wakati huo huo Marekani na Kenya walikubaliana mikataba ya jumla ya dola Milioni 900.

Bw Trump alikaribisha pendekezo lililowasilishwa na kampuni ya ujenzi kutoka Marekani ya Bechtel Corporation kutaka kupewa kandarasi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Mataifa yote mawili yalikubaliana na kuendelea na mashauriano zaidi ili kuafikiana kuhusu ufadhili wa ujenzi huo.

Mbali na hayo viongozi hao wawili walijadiliana pia kuhusu safari za ndege za moja kwa moja kutoka Nairobi hadi New York zitakazoanza mwezi Oktoba mwaka huu na kukubaliana kwamba safari hizo za ndege zitaimarisha zaidi utalii na biashara kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Rais Kenyatta ni kiongozi wa tatu kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara kukaribishwa Ikulu ya White House na kufanya mazungumzo na Rais Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.