Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Makundi hasimu kutia saini mkataba wa mwisho Jumatatu Sudan Kusini

media Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (katikati) anashikilia mkono wa hasimu wake Riek Machar kabla ya kutia saini makubaliano huko Khartoum Agosti 5, 2018. Kenya Presidential Press Service/Handout via REUTERS

Mkataba wa mwisho wa amani nchini Sudan Kusini unatarajiwa kutiwa saini Jumatatu ijayo, jijini Khartoum nchini Sudan. Mkataba huu unaeleza kuachiliwa huru kwa wafungwa, utoaji wa misaada ya kibinadamu na kuundwa kwa serikali ya mpito ndani ya miezi minne.

Waziri wa Habari Michael Makuei ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa mazungumzo yanayoendelea kwa sasa yanakwenda vizuri.

Bw. Michael Makuei amesema, pande hasimu nchini humo zimefikia mwafaka kuhusu mswada wa mkataba wa mwisho wa amani, ambao unatarajiwa kusainiwa Agosti 27, huko Khartoum.

Amesema mazungumzo ya sasa yanahusu masuala ambayo hayajatatuliwa ya kugawana madaraka na mipango ya usalama.

Naye Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom  ametaka pande zote kushughlulikia kwa kikamilifu suala la usalama katika mkataba huo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana