Pata taarifa kuu
BURUNDI-HAKI

Mwanaharakati wa haki za binadamu ahukumiwa miaka mitano jela Burundi

Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Burundi amehukumiwa kifungo cha miaka mitano, akishtumiwa kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi kwa niaba ya shirika lililopigwa marufuku na serikali, Aprodh, duru rasmi zimebaini.

Kiongozi wa shirika la haki za binadamu na wafungwa, Aprodh, Pierre-Claver Mbonimpa.
Kiongozi wa shirika la haki za binadamu na wafungwa, Aprodh, Pierre-Claver Mbonimpa. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo ulitolewa siku ya Jumatatu na mhakama mjini Bujumbura, kwa mujibu wa chanzo cha mahakama ambacho hakikutaja jina.

"Nestor Nibitanga kwa muda mrefu alikua akisimamia ofisi yetu huko Gitega" (katikati mwa nchi), kiongozi wa shirika linalotetea haki za binadamu na za wafungwa (Aprodh), Pierre-Claver Mbonimpa aliye uhamishoni ameliambia shirika la habario la AFP. Shirika hili kuuu linalotetea haki za binadamu na za wafungwa nchini Burundi, lilipigwa marufu na utawala wa Pierre Nkurunziza tangu kuanza kwa mgogoro wa Burundi mnamo mwaka 2015.

"Alihukumiwa siku ya Jumatatu asubuhi na Mahakama ya Mukaza (Mahakama ya mwanzo ya Bujumbura) kifungo cha miaka mitano kwa kutoa taarifa kuhusu haki za binadamu wakati Aprodh ilifutwa na serikali kwenye orodha ya mashirika yaliyosajiliwa nchini Burundi, "ameongeza Bw Mbonimpa.

Mwanasheria wa Nestor Nibitanga, Fabien Segatwa, amethibitisha hukumu hiyo kwa shirika la habari la AFP.

Nestor Nibitanga alikamatwa Novemba 21, 2017 na idara ya upelelezi (SNR) katika mji wa Gitega, kabla ya kupelekwa katika jela kuu la Rumonge (kusini magharibi mwa nchi) ambapo alizuiliwa tangu wakati huo.

"Serikali inaendelea na ukandamizaji wake dhidi ya mashirika ya kiraia lakini hata hivyo, hatukutarajia chochote kutoka mahakama ambayo inaendeshwa na serikali," Bw Mbonimpa ameliambia shirika la habari la AFP.

"Angalau hakuteswa au kuuawa kama wanaharakati wengine au wanasiasa wa upinzani wanaokamatwa na utawala, hata kama amefanyiwa unyonge kwa kuhukumiwa kifungo hicho" ameongeza Mbonimpa, ambaye aliponea kuuawa kwa risasi mnamo mwezi Agosti 2015.

Wanaharakati wengine wa haki za binadamu nchini Burundi wamehukumiwa tangu kuzuka kwa mgogoro nchini humo mwaka 2015.

Miongoni mwao ni Germain Rukuki, alihukumiwa kifungo cha miaka 32 mwezi Aprili kwa kuchochea "uasi", kwa sababu ya uanachama wake wa moja ya mashirika ya kiraia yaliyoitisha maandamano dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza mwaka 2015.

Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania kwa muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais aliibuka msindi mwaka 2015

Mwanzoni mwa mwezi Juni, Nkurunziza, mwenye umri wa miaka 54, alitangaza kuwa hatowania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 ingawa Katiba mpya inayomruhusu rais kusalia madarakani hadi mwaka 2034, ilipitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.