Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 23/04 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 22/04 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
E.A.C

Burundi yatangaza muda wa mwisho wa kutumia mifuko ya plastiki

media Kutokana kusudio hilo, serikali imetangaza kutoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hiyo na kujikita kwenye utengenezaji wa vifungashio mbadala. © RFI/Altin Lazaj

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametoa amri inayopiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini humo na kutoa muda wa mwisho wa kutumia mifuko hiyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu, kulingana na agizo la rais.

Kwa mujibu wa amri hiyo iliyosainiwa na Rais Nkurunziza utengenezaji, uagizaji, kuhifadhi, uuzaji na matumizi mengine ya mifuko ya plastiki vitapigwa maarufuku kufikia kipindi hicho.

Aidha amri hiyo itatoa ruhusa maalum ya mifuko ya plastiki na malighafi nyingine za plastiki kutumika katika huduma za ufungishaji dawa katika viwanda nchini humo kwa lengo la kukabiliana na uaharibifu wa mazingira

"Kipindi cha miezi 18 kinatolewa, kuanzia baada rais kutia saini nakala hii, ili kuweza kuuza na kutumia mifuko ya plastiki iliyokuwa imehifadhiwa na ile ambayo ilikua iliagizwa nje ya nchi," nakala hiyo imebaini.

Lakini mifuko ya plastiki, vifaa vya plastiki vinavyotumiwa katika huduma za matibabu, katika viwanda na maduka ya dawa" vitaendelea kutumiwa kwa masharti, imeongeza nakala hiyo.

Nchi nyingine za Afrika tayari zimeanza kupikabiliana na uchafuzi wa vifaa na mifuko ya plastiki, kama vile Morocco, Rwanda na Kenya, ambazo zilipiga marufu matumizi ya mifuko ya plastiki.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana