Kigwangala, alijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea mkoani, Manyara Kakazini mwa Tanzania, akiwa njiani kuelekea Dodoma.
Akizungumza katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli amesema serikali yake iko bega kwa bega na viongozi hao ambao wamepata ajali wakiwa wanalitumikia taifa.
Katika ajali hiyo Ofisa wa Habari, katika Wizara ya maliasili na utalii, Hamza Temba alipoteza maisha na anazikwa leo kijijini kwao, Hai Mkoani Kilimanjaro.
Viongozi mbalimbali wa kisiasa nchini tanzania wakimwemo Wabunge, Mwigulu Nchemba, Peter Msigwa, Zitto Kabwe wameandika kupitia mitandao ya kijamii wakimtakia kheri waziri Kigwangala ambaye ni mbunge katika Jimbo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.
Katika miezi ya karibuni Tanzania imekumbwa na matukio ya ajali za barabarani katika mikoa ya Mbeya, Kigoma, ajali ambazo zimegharimu maisha ya raia na mali zao.