Pata taarifa kuu
KENYA-RUSHWA-UCHUMI

Vita dhidi ya rushwa yazua wasiwasi Kenya

Serikali ya Kenya imeendelea kuwashughulikia viongozi mbalimbali wanaoshtumiwa rushwa nchini humo. Makumi ya washtumiwa tayari wanakabiliwa na mashitaka yanayohusiana na kashfa hiyo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) na kiongozi mkuu wa upinzani, Raila Odinga. ©SIMON MAINA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi ambao sasa wameanza kukabiliwa na mkono wa sheria ni maafisa waandamizi wa shirika la kusambaza umeme, Kenya Power.

Kesi kuhusiana na rushwa zimeendelea kushika kasi katika miezi ya hivi karibuni nchini Kenya, nchi inayoendelea kiuchumi, lakini inadhoofiswa na utamaduni wa rushwa na ubadhirifu, vitendo ambavyo rais Uhuru Kenyatta aliahidi kutokomeza.

"Tutarejesha fedha zote zilizoibwa. Hakutakuwa na msamaha kwa weziwezi. Siku zao zinahesabiliwa. Watakamatwa, wafunguliwe mashitaka na wafungwe," rais Kenyatta alisema mwishoni mwa mwezi.

Rais Uhuru Kenyata alitangaza kuwa rushwa ni tishio la usalama wa taifa.

Mnamo mwaka 2017, Kenya ilichukua nafasi ya 143 kati ya 180 katika ripoti ya kila mwaka ya shirika la Transparency International kuhusu rushwa.

Uchunguzi unalenga shirika la kusambaza umeme la Kenya Power unahusu ununuzi wa transoma za umeme zenye thamani ya dola milioni 4ambazo zilikutwa ni mbovu na haziwezi kutumika.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ken Tarus, aliyefutwa kazi, ni miongoni mwa viongozi wa naokabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.