Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA-USALAMA-HAKI

Yoweri Musevini kuwania muhula wa sita katika uchaguzi wa urais Uganda

Mahakama nchini Uganda imemruhusu rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni, mwenye umri wa miaka 73, kuwania muhula wa sita katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka 2021.

Upinzani unadai kuwa nia ya Museveni ni kusalia madarakani milele.
Upinzani unadai kuwa nia ya Museveni ni kusalia madarakani milele. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Januri maka huu, rais Museveni madarakani kwa miaka 31 sasa, aliidhinisha sheria inayofuta ukomo kwa mgombea mwenye umri wa miaka 75 kuwania katika uchaguzi wa urais, na hivyo kusababisha hasira upande wa upinzani ambao ulishtumu mbino za kutaka "kukaa madarakani milele".

Baada ya hatua hiyo muungano wa vyama vya upinzani ulikwasilisha malalamiko yako mahakamani.

Wengi wa majaji wa Mahakama ya Katiba waliokutana katika kikao maalum huko Mbale, karibu kilomita 225 mashariki mwa Kampala, waliamua kupitisha sheria hiyo inayofuta ukomo kwa wagombea wenye umri wa miaka 75 kuwania urais.

Sheria iliyopitishwa na Museveni pia ilirejesha ukomo kwa idadi ya mihula kwa rais, iliyokua ilifutwa mnamo mwaka 2005.

Museveni, ambaye alichukua hatamu ya uongozi wa nchini mwaka 1986 akiwa mkuu wa jeshi la waasi, aliwahi kusema kuwa viongozi ambao "wanakaa muda mrefu madarakani" wanakuza chuki na kusababisha matatizo barani Afrika.

Lakini wakati alipokuwa mgombea urais kwa muhula wa tano mwaka wa 2016, alisema muda hauajafika yeye kuchia ngazi, akisema bado ana kazi nyingi za kufanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.