Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Askari watatu wapigwa mawe hadi kufariki nchini Uganda

Askari watatu wa Uganda wameuawa kwa kupigwa mawe na watu wenye hasira karibu na mpaka na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kushtumiwa kuwa wahalifu na wakazi wa eneo hilo, polisi imesema katika taarifa yake.

Askari wa Uganda wakipiga doria katika msito ambapo wanadaiwa kujificha waasi wa LRA mwezi Aprili 2012.
Askari wa Uganda wakipiga doria katika msito ambapo wanadaiwa kujificha waasi wa LRA mwezi Aprili 2012. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Askari wetu watatu wameuawa na umati wa watu na uchunguzi unaendelea ili kujua mazingira ambamo waliuawa," Peter Debele, afisa mwandamizi nchini Uganda ameliambia shirika la habari la AFP.

"Silaha tatu zimeokotwa eneo la shambulio na watu nane wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya askari hao," aliongeza.

Askari hao ni wa kikosi cha ulinzi wa eneo la mpaka wa Uganda huko Vurra.

Mapema mwaka huu, serikali ilipiga marufu raia kuvaa nguo zinazofanana na sare za vikosi vya usalama na ulinzi kwa sababu wahalifu wengi wanavaa sare za jeshi.

Askari walikamatwa karibu kilomita 8 kutoka eneo hilo la mpaka na kuhojiwa na wakazi. walikubali kukabidhi silaha zao, lakini umati wa watu uliwapiga mawe hadi kufariki, huku wakibaini kwamba walikua walikuja kuiba," amesema Peter Debele.

Msemaji wa polisi wa Uganda katika mkoa huo, Josephine Angucia, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mmoja wa askari waliouawa alikuwa kamanda wa kitengo kilichowekwa kwenye kituo cha mpaka, Kaporali Julius Kobum.

"Tunawatolea wito raia kutojichukulia sheria mkononi wanapokabiliwa na tatizo, wangelipaswa kuripoti tukio hilo kwa polisi," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.